TPDC: Nusu ya Tanzania ina mafuta na gesi
Dodoma. Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limesema nusu ya ardhi ya Tanzania inaweza kuwa na mafuta au gesi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Mei 29, 2019 jijini Dodoma, Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo, Kapuulya Musomba amesema utafiti wa mafuta na gesi upo katika theluthi moja tu katika kipindi cha miaka 50 ya uwepo wa taasisi hiyo.
Ametoa maelezo hayo ikiwa ni utangulizi wa miaka 50 ambayo wataazimisha kesho Jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Musomba amesema tangu walipogundua uwapo wa gesi mwaka 1974, hali ya matumizi ya gesi nchini haijawa ya kuridhisha kama walivyotarajia.
Mkurugenzi huyo amesema bado wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ya kusimamisha uzalishaji katika mwaka 2000 huku Shirika likiwa na mzigo wa madeni.
Kiongozi huyo amesema tangu mwaka 2015, TPDC ilitengenezewa sheria ya kufanya biashara, hivyo wamejipanga kwa ajili ya biashara nchini.
Amesema wamejipanga kwa ajili ya kufanya biashara na ndiyo maana wamekuwa wakipunguza madeni ambayo waliyarithi ndani ya Shirika.
Comments
Post a Comment