Sakata la Nyalandu na wenzake ngoma mbichi


Singida/Dar. Sakata la kukamatwa kwa aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu na wenzake wawili bado halikawekwa wazi baada ya jana kuripoti Polisi mkoani Singida ambako walichukuliwa maofisa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) kuhojiwa na kisha kuachiwa kwa dhamana.

Waziri huyo wa zamani wa Maliasili na Utalii ambaye kwa sasa ni kada wa Chadema, alikamatwa Jumatatu na maofisa wa Takukuru katika Kata ya Itaja Singida Kaskazini, wakituhumiwa makosa mawili ya rushwa na kuendesha mkutano usiokuwa na kibali.
Jana, watuhumiwa hao walitekeleza agizo la kuripoti katika Kituo cha Polisi cha Kati Singida mjini, walikotumia nusu na kabla ya kutakiwa kurudi kesho.
Kabla ya kuruhusiwa kuondoka, makada hao wa Chadema walichukuliwa na maofisa wa Takukuru ambako walihojiwa kabla ya kuachiwa kwa dhamana ya Sh5 milioni kila mmoja.
Wakati Kamanda wa Takukuru, Mkoa wa Singida, Joshua Msuya akisema watuhumiwa hao hawakuohojiwa jana ila wamewapangia kuripoti siku nyingine, Nyalandu alisema wamehojiwa na kutakiwa kurejea tena Juni 19.
“Hatujawahoji ila wamekuja na tumewapatia utaratibu wa kuripoti siku nyingine, siwezi kusema ni lini kwa sababu ni taratibu za kiofisi,” alisema Msuya.
Nyalandu alisema hadi sasa hawajaelezwa makosa yao, “inashangaza sana lakini ninawaomba makamanda wote (wanachama wa Chadema) kuwa na utulivu, kutolipa ubaya kwa ubaya ila walipe ubaya kwa wema,” alisema Nyalandu.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Singida, Shaaban Lyimo alisema walikamatwa wakiwa katika mkutano wa ndani wa utekelezaji wa agizo la Msajili wa Vyama vya siasa linaloagiza kufanya uhakiki wa wanachama.
Juzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike aliwaeleza wanahabari kuwa, jeshi hilo halina shida yoyote na watuhumiwa hao ila Takukuru waliomba nafasi ya kuwahifadhi.

Comments

Popular Posts