Mbunge Azungumzia Presha ya Mnyika na Sugu 2020

Mbunge Azungumzia Presha ya Mnyika na Sugu 2020

Mbunge wa Serengeti (CCM) Rioba Chacha amesema kuwa kama ikitokea mtu yeyote anapingana na maono ya Baba wa taifa Mw. Julius Nyerere, basi atakuwa amelaaniwa hivyo kinachoendelea kwa kambi ya upinzani ni presha ya kukosa nafasi uchaguzi ujao wa 2020.

Chacha ametoa kauli hiyo wakati akichangia bajeti ya wizara ya Nishati Bungeni ambapo amewataka viongozi wa upinzani kuunga mkono kile kinachofanywa na serikali na sio kukosoa kila kitu.

"Unajua mimi pia nimetokea kule (CHADEMA) ili mtu uchangie bungeni lazima utumie kile kitu cha Tarime (Bangi), hivyo sio wao ni laana hizo hakuna mtu mzalendo nchi hii kumzidi hayati baba wa taifa", amesema Chacha.

"Unadhani mtu kama Mnyika na Sugu watarudi bungeni, watapitishwa na nani? Kwahiyo muwasamehe tu michango yao ni hofu ya uchaguzi mkuu wa 2020", ameongeza Chacha.

Hayo yamejiri baada ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2019/20 ya shilingi trilioni 2.142 . Kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 1.44 zimeelekezwa katika mradi wa kuzalisha umeme katika Mto Rufiji wa Stiegler’s Gorge.

Mbali ya mradi huo, bajeti hiyo ambayo imeongezeka kutoka shilingi trilioni 1.69 mwaka 2018/19, inakwenda kugharamia miradi mingine mikubwa miwili ya kimkakati ambayo yote itagharimu asilimia 95 ya bajeti nzima ya wizara hiyo. 

Hiyo ni mradi kabambe wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu shilingi bilioni 363.11 na mradi wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi I Extension MV185 shilingi bilioni 60.

Comments

Popular Posts