Magufuli aendesha harambee
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli ameendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa msikiti huku wachungaji wa madhehebu mbalimbali wakishiriki shughuli hiyo.
Katika harambee hiyo zaidi ya Sh20 milioni zilikusanywa ikiwa ni ahadi na fedha taslimu.
Rais Magufuli alifanya harambee hiyo leo Jumanne Aprili 30 mara baada ya kumaliza hotuba yake aliyoifanya katika viwanja vya Mwakangale wilayani Kyela jijini Mbeya ikiwa ni sehemu ya ziara yake inayoendelea mkoani humo.
“Kuna Sheikh hapa aliomba mchango wa ujenzi wa msikiti, yupo wapi nitakukabidhi Sh5 milioni hebu njoo hapa, na hii fedha isiende ikapotea ikatumike kwa ajili ya kujenga msikiti siku nitakapokuja nitakuja kupaona, mawaziri wangu wote njooni hapa mseme mnachangia shilingi ngapi,” amesema Magufuli.
Pamoja na mawaziri, pia viongozi mbalimbali waliokuwa kwenye ziara hiyo ya Rais Magufulu walichangia wakiwamo maaskofu na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Kyela lililochangia Sh240,000.
Comments
Post a Comment