Rais Uhuru Kenyatta ampongeza Peter Tabichi kwa kutwaa tuzo ya mwalimu bora duniani, asimulia alivyopanda ndege kwa mara yake ya kwanza (+video)
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amempongeza mwalimu Peter Tabichi wa nchi hiyo ambaye ameshinda Tuzo ya Dunia ya Mwalimu Bora kwa mwaka huu 2019.
Kenyatta amesema tuzo hiyo inajaribu kueleza namna ambavyo uadilifu na uchapakazi “unalipa”.
Kwa ushindi wa tuzo hiyo, mwalimu Tabichi amepatiwa Dola milioni 1.
Kenyatta amesema tuzo hiyo inajaribu kueleza namna ambavyo uadilifu na uchapakazi “unalipa”.
Kwa ushindi wa tuzo hiyo, mwalimu Tabichi amepatiwa Dola milioni 1.
Kwa upande wake mwalimu, Peter Tabichi amesema kuwa ushindi huo ni wa kila mmtu ”Huu ushindi ni wa kila mtu, barani Afrika, wanafunzi na watu wengine ambao wamenipa ushirikiano.”
Peter Tabichi ni mwalimu wa kwanza kutoka katika bara hili la Afrika kuweza kutwaa tuzo hiyo ambapo kwa upande wake amesema anafuraha tele.
”Nipo na furaha tele, kwa sasa hivi naweza kusema kwamba siamini, hata watu wengine wanasema hivyo hivyo hawaamini lakini kadri unavyopitia changamoto ndivyo unavyo karibia yale mazuri.”
”Nilikuwa sifahamu kama kuna mashindano kama haya, lakini kuna mtu alikuwa anaona kile ambacho nafanya akanishauri nishiriki kwenye haya mashindano, nikajisajili kwa kutuma barua ambayo inaambatana na kile ambacho ninafanya kama ushahidi.”
Peter Tabichi ni mwalimu wa sayansi kutoka rural Kenya ambapo ametangazwa kuwa mwalimu bora duniani nchini Dubai na kukabidhiwa kitita cha dola za Kimarekani milioni moja ambazo ni sawa na pauni laki 760,000.
Ushindi wake unatokana na kutumia 80% ya mshahara wake kuwasaidia wanafunzi wenyeshida mbalimbali wa Keriko Mixed Day Secondary School iliyopo Pwani Village, Nakuru na kubakiwa na 20% pekee kumsaidia kwenye matatizo yake binafsi
Comments
Post a Comment