Pascal wa BSS arejea Tz kutoka India kwenye matibabu, Daktari asema ataendelea kutumia mipira kutoa haja ndogo (+video)
Baada ya kukaa India kwa takribani mwezi mmoja akipatiwa matibabu, hatimaye mshindi wa BSS 2009, Pascal amerejea nchini akiwa na afya njema ukilinganisha na alivyoondoka.
Pascal amewashukuru Watanzania na RC Makonda kwa kufanikisha safari hiyo na gharama za matibabu.
Kwa upande mwingine, Daktari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Steven Nicolaus amesema kuwa Pascal alifanyiwa upasuaji wa kibofu na ataendelea kutumia mipira kutoa haja ndogo kwa siku 30, mpaka hali yake itakapokuwa sawa.
Comments
Post a Comment