Mahakama Kuu ya Dodoma imetupilia mbali ombi la Nassari la kufungua kesi dhidi ya Spika wa Bunge (+ Video)
Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imetupilia mbali ombi la Joshua Nassari(CHADEMA) la kufungua kesi ya msingi dhidi ya Spika wa Bunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kupinga kuvuliwa Ubunge.
Nassari alifungua shauri hilo akidai kuonewa kwani alituma barua kwa ofisi ya Spika wa Bunge akiwajulisha kuhusu kutokuwepo kwake.
Kwa maana hiyo Mahakama imekubaliana na uamuzi wa Spika wa Bunge la Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, wa kufuta nafasi ya ubunge kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nasari.
Comments
Post a Comment