BBC na VOA zafungiwa kurusha matangazo Burundi
Serikali ya Burundi kupitia Baraza na Mawasiliano la Taifa (CNC) nimezuia matangazo ya Shirika la habari la nchini Uingereza(BBC) na Redio za Shirika la Habari la nchini Marekani(VOA) mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo.
Inaelezwa kuwa sababu kubwa ya kufungiwa kwa matangazo ya Mashirika hayo ni kutokana na Serikali ya Burudi kuvishutumu kutoheshimu sheria na kutokuwa na utashi wa Kiuandishi
CNC imesema “Kuzuiliwa kutangaza kwa VOA kunaendelea hadi itakapotangazwa vinginevyo, hivyo basi ni marufuku Mwanahabari yeyote raia wa Burundi au Mgeni anayeishi Burundi kuripoti kwa VOA(Voice of America)
BBC inashutumiwa kwa kuongeza mafuta kwenye video inayoonesha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ukifanywa na Afisa Usalama wa Burundi, video ambayo Serikali imesema kwa kiasi kikubwa imetengenezwa
Aidha, VOA inashutumiwa kwa kuendelea kuajiri Wanahabari ambao Serikali iliwakataza wasiwaajiri kwani Wanhabari hao natakiwa kujibu mashtaka yao ya kudaiwa kuhusika katika vurugu za uchaguzi zilizotokea mwaka 2015
Comments
Post a Comment