Trump, Kim Jong Un uso kwa uso Vietnam
Rais wa Marekani, Donald Trump atakutana kwa mara ya pili na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un saa chache zijazo nchini Vietnam kujadili kuhusu mpango wa kuondoa silaha za kinyuklia katika Rasi ya Korea.
Kim Jong Un alisafiri tangu juzi kwa treni iliyokuwa na silaha nzito akipitia China na leo atakuwa nchini humo kukutana na swahiba wake huyo ambaye alikuwa hasimu miaka miwili iliyopita.
Rais Trump ameandika kwenye mtandao wake wa Twitter kuwa hakuna haja ya kuwaharakisha Korea Kaskazini kuachana kabisa na mpango wa makombora ya nyuklia, na kwamba anafurahishwa na hatua ya kusitisha majaribio ya makombora hayo.
Kauli hiyo imetokana na mkanganyiko wa ripoti za vyombo vya habari kuhusu makubaliano ya mwaka jana kati ya viongozi hao, ambapo imekuwa ikiripotiwa kuwa walikubaliana Korea Kaskazini kuteketeza vinu vyake vya kinyuklia. Hata hivyo, ripoti ya mazungumzo yao inadaiwa kuwa ni tofauti kwamba walichokubaliana ni kusitisha majaribio na kuanza mchakato wa kutokomeza silaha za nyuklia katika rasi yote ya Korea (Kusini na Kaskazini).
Jana, Trump alitweet akiwakosoa watu ambao amedai wamekuwa wakitoa taarifa za uongo wakidai hamheshimu Kim Jong
“Ripoti zote za uongo kuhusu heshima yangu kwa Korea Kaskazini. Kim Jong Un na mimi tutajaribu iwezekanavyo kupata matokeo kuhusu kuachana na nyuklia. Kisha kuifanya Korea Kaskazini kuwa taifa lenye nguvu kiuchumi. Ninaamini China, Urusi, Japan na Korea Kusini watakuwa msaada sana,” alitweet.
Hotel ya Metropole, sehemu ambayo Kim Jong Un na Donald Trump wanakutana
Mwaka jana baada ya mkutano wao, Trump alieleza kuwa amekuwa rafiki mkubwa wa Kim Jong Un tangu akutane naye kwakuwa amebaini ni mtu makini na mwenye uwezo mkubwa. Alisema kuwa amekuwa akimuandikia barua nzuri.
“Ameniandikia barua nzuri sana. Nimezipenda. Urafiki wetu umekuwa mkubwa, tunapendana,” Trump alisema.
Mkutano huu ni wa pili wa kihistoria baada ya ule wa kwanza walioufanya nchini Singapole mwaka jana. Viongozi hawa wamekuwa wa kwanza katika historia ya nchi hiyo kuwa wakuu wan chi waliokutana wakiwa madarakani.
KWA HABARI ZA MICHEZO PAKUA APP YETU YA MICHEZO SASA
Comments
Post a Comment