Homa ya uchaguzi mkuu yaanza kupanda Bungeni



Ikiwa imebaki miezi kadhaa kuelekea uchaguzi mkuu, baadhi ya wabunge wameonyesha kuwa na hofu juu ya kuchelewa kwa marekebisho ya daftari la wapiga kura.

Mbunge wa viti maalumu (Chadema), Cecilia Pareso leo aliuliza swali Bungeni kutaka kujua ni namna gani katika kipindi kilichobaki Serikali inaweza kutoa haki kwa Watanzania wenye sifa ya kujiandikisha ili watumie haki yao mwakani kupiga kura.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na wenye Ulemavu, Anthony Mavunde  amesema: "Mheshimiwa Spika, mchakato wa kuboresha daftari la wapigakura ulianza mwezi Agosti 2018, kwa kuhuisha kanzidata ya daftari la kudumu la wapigakura na kuboresha mifumo ya uandikishaji na utunzaji wa kumbukumbu za daftari."

Mavunde amesema kwa mujibu wa kifungu cha 15(5) cha Sheria ya Uchaguzi, sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iko katika hatua za mwisho za kufanya maandalizi ya uboreshaji wa daftari kwa majaribio katika baadhi ya mikoa. 


==>>Msikilize hapo chini



                    KWA HABARI ZA MICHEZO PAKUA APP YETU YA MICHEZO SASA


Comments

Popular Posts