Ester Matiko atoa bati 1324 akiwa gerezani
Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Mhe Esther N. Matiko ameamua kununua Bati zipatazo 1324 kwa ajili ya kuezeka Vyumba vya Madarasa 21, Ofisi 3 za Walimu na Vyoo 2 vyenye jumla ya Matundu 16. Mhe Esther N. Matiko ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini yuko Gerezani kwa muda wa siku 72 tangu kufutiwa dhamana na Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es salaam.
Mhe Esther N. Matiko ameamua kuchukua maamuzi hayo baada ya idadi kubwa ya wanafunzi wa Darasa la 7 waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza wapatao *2046* kati ya hao ni Wanafunzi *416* tu walipata nafasi ya kuanza kidato cha kwanza na Wanafunzi *1630* wamekosa nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza sababu tu ya upungufu wa vyumba vya Madarasa katika Shule za Sekondari Tarime Mjini.
Matiko ameamua kununua Bati hizo kupitia fedha za Mfuko wa Jimbo ambazo ni Tsh *31,000,000/=* ili kuwezesha uezekaji wa Madarasa hayo na kutoa fulsa kwa watoto hao kupata Haki yao ya Msingi ya kupatiwa Elimu.
Bati hizo zilizonunuliwa na Mhe Bashiri Abdalah Suleiman (Sauti) ambaye amekaimu nafasi ya Mhe Matiko mgawanyo wake ni kama ifuatavyo.
(1) Shule ya Sekondari Sabasaba Mabati 440 kuezeka Madarasa 7 na Ofisi 1 ya Walimu na Matundu 8 ya vyoo
(2) Shule ya Sekondari Nyamisangura Mabati 240 kuezeka Madarasa 4 na Ofisi 1 ya Walimu
(3) Shule ya Sekondari Nyandoto Mabati 120 kuezeka Madarasa 2
(4) Shule ya Sekondari Kenyamanyori Mabati 142 kuezeka Madarasa 2
(5) Shule ya Sekondari Tagota Mabati 250 kuezeka Madarasa 4 na Ofisi 1 ya Walimu na Choo cha Matundu 8
(6) Shule ya Sekondari Nkende Mabati 190 kuezeka Madarasa 3
(7) Shule ya Sekondari Rebu Mabati 60 kuezeka Darasa 1.
Kukamilika kwa vyumba hivyo vya Madarasa kutakuwa kumetoa fulsa kubwa sana kwa Wanafunzi walioachwa kujiunga na elimu ya Sekondari ikiwa ni haki yao ya Msingi.
Ofisi ya Mbunge Jimbo la Tarime Mjini inapenda kuwaambia Wananchi wote wa Tarime Mjini kuwa Bati hizo zote zilizopelekwa kwenye Shule wanazojenga zimetolewa na Mhe Esther N. Matiko na sio Mtu yeyote .
Mhe Esther N. Matiko anapenda kuwahasa Wananchi wote na watendaji waliopokea Bati hizo zitumike kwa Matumizi yaliyopangwa tu na sio jambo lingine.
Comments
Post a Comment