Watanzania watakiwa kula kilo 50 za nyama kwa mwaka
Bodi ya nyama Tanzania (TMB) imewataka wananchi kula nyama bora na salama kwa kiwango kinachotakiwa ambacho ni wastani wa kilo 50 kwa mtu mmoja kila mwaka.
Hayo yamesemwa na kaimu msajili wa bodi ya nyama Tanzania, Imani Sichazwe leo Jumatano Oktoba 31 wakati akizungumza na wandishi wa habari Jijini Dar es salaam.
Sichazwe amesema Tanzania ni nchi ya tatu kwa wingi wa mifugo ikitanguliwa na Ethiopia pamoja na Sudani lakini ulaji nyama umekuwa wa kiwango cha chini chenye wastani wa kilo 15 kwa kila mmoja.
“Nchi yetu inakadiriwa kuwa na N’gombe takribani milioni 30.5, Mbuzi milioni 18.8, Kondoo million 5.3, Kuku wa asili milion 38.2, Kuku wa kisasa million 36.5, Nguruwe million 1.9 na Punda 595,160.
Aidha amesema nyama ni zao la biashara na chakula linalotokana na mifugo iliyochinjwa kuliwa baada ya kukaguliwa na kuthibitishwa kuwa salama kwa matumizi.
Application ya CCM NEWS Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
Comments
Post a Comment