Tatizo si kukamata mashoga- RC Mwanri
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwanri amesema kuwa wakuu wake wa Wilaya wameanzisha utaratibu maalumu wa kuwakagua wageni wanaoingia mkoani humo kwa lengo la kutokomeza biashara haramu ikiwemo ya ukahaba, na madawa ya kulevya.
Mwanri ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na kituo kimoja cha Radio jijini Dar es salaam alipokuwa akiwasilisha mpango wa mkoa wake wa kuandaa jukwaa maalumu litakalohusu uwekezaji katika mkoa huo.
Mwanri aligusia suala la biashara ya ukahaba mkoani kwake ambapo amesema kuwa wengi miongoni mwa watu hao wamekuwa wakitokea mikoa mingine hasa Dar es salaam na kuingia mkoani humo.
“Ukienda kwenye nyumba za wageni za Tabora, utashangaa kumuona mtu anatakata tu lakini hujui biashara anayofanya, nimewagiza wakuu wangu wa wilaya wakipita watu ambao hawajulikani wakaguliwe kazi gani wanafanya,”amesema Mwanri.
Aidha, kuhusiana na suala la elimu, Mwanri amesema kuwa mpango wake ni kuhakikisha kila nyumba ya mkazi wa Tabora inafanikiwa kutoa mhitimu wa elimu ya Chuo Kikuu.
Hata hivyo, ameongeza kuwa kama mtu akitaka wananchi wake wawe na vifaa waelemishe watu wake, asiwadharau, mpango walionao ni kutoa wahitimu wa chuo kikuu katika kila nyumba ya mkazi wa Tabora, ambapo amesema hata bibi kizee mwenye miaka 80 atapata degree (Shahada ya kwanza) lakini ndani ya miaka 30 ijayo kama atakuwepo ndio maana wanawekeza kwa watoto.
Application ya CCM NEWS Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
Comments
Post a Comment