Serikali Ya Tanzania Yaanza Mazungumzo Na Ujerumani Ya Mgao Wa Mapato Yatokanayo Na Mjusi Mkubwa ‘Dinosaur’ Kupitia Watalii
Serikali ya Tanzania kupitia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga imesema ipo kwenye hatua za awali za mazungumzo na Serikali ya Ujerumani kuona jinsi itakavyofaidika na mapato yatokanayo na utalii kupitia mabaki ya Mjusi mkubwa ‘’Dinosaurs ambaye ni kivutio cha kikubwa cha utalii katika jumba la Makumbusho nchini Ujerumani
Mjusi huyo kwa jina la kitaalamu anaitwa Dinosaur ambapo mabaki yake yalivumbuliwa miaka 100 iliyopita katika eneo la Tendaguru mkoani Lindi, yalikusanywa na kupelekwa nchini Ujerumani ambako wataalamu waliyaunda na kisha kuyaweka kwenye Makumbusho hiyo.
Amesema lengo la mazungumzo hayo ni kutaka kujua kiasi gani cha mapato yanayokusanywa na namna gani wanavyoweza kugawana mapato hayo yatokanayo na watalii kupitia mjusi huyo baina ya Serikali hizo mbili.
Amesema mwelekeo wa mazungumzo hayo yaitapelekea Serikali ya Tanzania kufanya uamuzi wa kumrudisha mjusi huyo au kumuacha kule kule lakini akiwa analiingizia pato taifa
Ameyabainisha hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na mIkakati ya Serikali ya kuendeleza vivutio vya utalii kwa mikoa ya Kusini.
Hata hivyo, Mhe.Hasunga amesema uamuzi wa kumrudisha mjusi huyo nchini utakuwa mgumu kwa vile sehemu kubwa ya mjusi huyo ameunganishwa unganishwa kwa kutumia vifaa maalumu.
Ameongeza kuwa kutokana na jinsi alivyounganishwa unganishwa na anakadiri wa kuwa na urefu wa mita 13.7 kwenda juu hivyo kumsafirisha itakuwa ngumu.
Katika hatau nyingine, Mhe Hasunga amesema hadi hivi sasa Serikali ya Ujerumani haijaweza kuweka bayana kiasi cha mapato yanayokusanywa kupitia Mjusi huyo licha ya kuwa Serikali hiyo imekuwa ikifadhili miradi mingi ya uhifadhi nchini.
"Tunaamini kuwa pesa wanazofadhili miradi mingi ya Uhifadhi imekuwa inatokana na makusany okupitia Mjusi huyo Mkubwa" amesema Hasunga
Hata hivyo,kuendelea kuwepo kwa masalia ya mjusi huyo katika Makumbusho hiyo kuna manufaa makubwa kwa vile anatambuliwa kuwa ni wa kutoka Tanzania,Hivyo ni Balozi
Application ya CCM NEWS Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
Comments
Post a Comment