RC Mnyeti Aongeza Chachu ya Ufaulu Wanafunzi Wilayani Kiteto.
Imeelezwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ameongeza chachu ya ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba, baada ya kuwatumbua walimu wakuu wa shule za msingi 28.
Mnyeti, emetajwa kuongeza ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba 2018, Wilayani Kiteto kutoka 59% mwaka jana hadi 69%.
Afisa elimu msingi wilaya ya Kiteto Bw. Emmanuel Mwagala alitaja sababu za ufaulu huo kuwa ni kutumbuliwa kwa baadhi ya walimu wakuu pamoja na jitihada kwa walimu wengine.
“Ziara ya mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti hapa Kiteto mwaka 2017 imeongeza chachu ya ufaulu kwa wanafunzi wa mwaka 2018 kwani kitendo cha kutumbuliwa walimu 28 kumeongeza jitihada kwa walimu wengine kufanya kazi zaidi”
Akizungumzia ufaulu huo mbele ya baraza la madiwani Kiteto Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Lairumbe Mollel (CCM) alisema shule ya msingi Boma Sidan imebeba Wilaya kwa kushika nafasi 54 Kitaifa.
Alisema mbali na shule hiyo pia shule la msingi Lalakir iliyoko kundi la wanafunzi chini ya 40 imeshika nafasi ya 3 Kitaifa kwa kufaulisha wanafunzi wa darasa la saba.
“Waheshimiwa madiwani, mwaka huu Wilaya ya Kiteto imefanya vizuri sana katika mtihani wa darasa la saba mwaka huu 69% tofauti na mwaka Jana 59% hivyo niwasihi tuzidi kuongeza jitihada”
Michael Lepunyati (CCM) Diwani wa kata ya Namelock alipongeza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kiteto Tamimu Kambona kwa kutoka ushirikiano katika maendeleo ya Elimu wikayani humo.
Application ya CCM NEWS Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
Comments
Post a Comment