kafulila afunguka kuhusu kurudi tena bungeni



Katibu Tawala Mkoa Songwe, David Kafulila amesema muda ukifika anaweza kuamua kama atawania nafasi ya Ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au kubaki kwenye nafasi yake ya ambayo aliteuliwa na Rais Magufuli. 

Kafulila amesema “suala la kugombea au kutogombea ubunge ni muda tu ila kwa sasa hivi nachoweza kuzungumza kwa sasa ni kwamba nafurahia, kufanya kazi. 

“Mimi nafanya kazi hadi saa tano za usiku, mimi nafanya kazi mpaka ziishe, sifanyi mpaka muda uishe, nafanya kazi kwa mapenzi na natakiwa nimalize, na sasa hivi kuna mambo mengi sana ambayo nimeyafanya mimi na Mkuu wa Mkoa nitakukaribisha uje kujionea”, ameongeza Kafulila. 

Hivi karibuni Kafulila alisema “kazi yangu ya utendaji hasa zama za Magufuli imekuwa nyepesi kwa mtendaji mwaminifu, na hasa ukiwa mtendaji ambaye hupendi rushwa, mi nafurahia sana nipo kwenye utendaji, ningekuwa kwenye ubunge ningependekeza lakini mimi kama mtendaji ninatakiwa kufanya maamuzi." 

Julai 28 mwaka huu Rais Magufuli alitangaza kuwateua baadhi ya makada waliokuwa wamehama kutoka upinzani na kujiunga na CCM kwa nia ya kumuunga mkono, akiwemo Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi, Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Mosses Machali  na David Kafulila kama Katibu Tawala wa Songwe.

            Application ya CCM NEWS Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi   
 

Comments

Popular Posts