CHADEMA Yazidi Kupukutika....Madiwani Wawili Wahamia CCM
Ngome ya Chadema wilayani hapa inazidi kuporomoka kufuatia madiwani wawili akiwemo makamu mwenyekiti kubwaga manyanga.
Ndani ya siku tatu toka amejivua nyadhifa zote ikiwemo ubunge, Marwa Ryoba na kuhamia CCM, madiwani watatu wameshajitoa hali ambayo inaonyesha wazi chama hicho kiko hatarini kupoteza halmashauri.
Waliojivua nyadhifa na kuthibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Juma Hamsini ni Pasto Maiso kata ya Ring'wani ambaye alikuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri kwa vipindi viwili.
Mwingine ni George Mahemba kata ya Magange ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Masinki kupitia Chadema.
Install Application ya CCM NEWS Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
Comments
Post a Comment