Sumaye: CCM Imepoteza Mwelekeo, Wananchi Wameichoka

Sumaye: CCM Imepoteza Mwelekeo, Wananchi Wameichoka

Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye amesema moja ya dalili za chama cha siasa kilichochokwa na wananchi ni  kutumia nguvu.

Sumaye ambaye ni mwenyekiti wa Chadema kanda ya Pwani ametoa kauli hiyo jana Alhamisi Agosti 30, 2018  wakati akimnadi mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Ukonga, Asia Msangi katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Gulu Kwalala.

Alisema CCM imechokwa na wananchi na kwa saa inachokifanya ni kung’ang’ania madarakani kwa kutumia nguvu.

“Kama unajiamini na wananchi wanakukubali kwa nini uwaonee wananchi, uwatishe kwa kila aina ya vitisho. Huko ni  kujilazimisha kuwa wananchi wanakukubali  wakati unawaziba midomo. Unawalazimisha kukubali unachokitaka,” alisema.

Amesema wanaopenda  mabadiliko ndani ya  Chadema, CUF na hata CCM,  huu ndio wakati wao wa kujipambanua na kuonyesha uwezo wao katika siasa kwa kufanya uamuzi sahihi.

“Hivi kweli hatuna akili kiasi hiki? Mtu tulimpa kura hapa hapa na ametutukana hadharani na bado tunampa tena” alihoji  Sumaye akimlenga mgombea wa CCM katika jimbo hilo, Mwita Waitara , ambaye awali alikuwa mbunge wa Ukonga kwa tiketi ya Chadema.


Comments

Popular Posts