Paul Makonda Hawezi Kutumbuliwa...Wanaomuombea Mabaya Watapata Tabu Sana



Mimi nasema kwa utamaduni wa viongozi wa CCM kujisahihisha ni jambo la kawaida, hata Mwl Nyerere aliwahi kuwafokea hadharani viongozi wengi tu wakiwemo akina John Malecela, Rashid Kawawa na wengine wengi lakini walipokemewa hakuwatupa kwa sababu walikuwa ni wapiganaji wake. Waliendelea kuwepo na mpaka leo ni miongoni mwa watu wenye heshima kubwa.

Paul Makonda ni kiongozi kijana, mchapakazi, mbunifu na jasiri. Sifa hizo hata Rais mwenyewe anazijua na amesema mara nyingi hadharani, na siamini kuwa anaweza kukubali kumuacha mpiganaji wake muhimu kama Makonda. Ndio maana kaamua kumsema hadharani ili ajirekebishe na aendelee na kazi na kwa kweli nionavyo mimi, Makonda ataendelea na kazi, hatamhamisha Dar es Salaam.

Bahati mbaya wengi ambao wanashangilia ni walewale wapinzani wa Serikali ya Rais Magufuli. Wanaona kuwa kikwazo chao cha Dar es Salaam kitaondoka. Maana tuwe wakweli Makonda Dar es Salaam kaishika na upinzani ni kama vile haupo. 
Kwa hiyo wale mnaoandika mipasho mkiwaaminisha watu kuwa Makonda atatumbuliwa mimi nawashauri achaneni na kampeni hiyo maana kwenye hili mmefeli.

Kwanza hizo fenicha zenyewe zilizoagizwa sio kwamba kuna makosa makubwa sana, ni kwamba Paul Makonda nadhani aliongozwa na ujana wake na hakuzingatia sheria, lakini fenicha zipo na Serikali ikiuza itapata fedha inazohitaji au itagawa kwa shule na mambo yatakuwa yaleyale. Hapa ni Makonda kaoneshwa kuwa anatakiwa kuzingatia sheria.

Imeandikwa na
Mwl. John Bacheleza 
Kinondoni.
Agosti 30, 2018

Comments

Popular Posts