Maaskofu 22 washiriki ibada ya mazishi ya Askofu Timanywa
Bukoba. Maaskofu 22 wanashiriki ibada ya mazishi ya Askofu mstaafu wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Nestor Timanywa itakayoongozwa na Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam Thadeus Ruwai'ichi.
Mazishi yanafanyika katika kanisa la Bikra Mariam, Mama Mwenye Huruma mjini Bukoba ambapo baada ya kuuaga mwili maaskofu na mapadri wameingia kanisani kwa maandamano.
Ndani ya kanisa ilipotengwa nafasi ya viongozi wa Serikali anaonekana mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti na baadhi ya wakuu wa wilaya.
Baadhi ya waumini wanafuatilia ibada hiyo wakiwa nje kwenye viwanja vya kanisa kupitia kwenye vipaza sauti na televisheni.
Marehemu Askofu Nestor Timanywa alifariki Agosti 28 mwaka huu wakati akitibiwa Hospitali ya rufaa ya Bugando Jijini Mwanza.
Comments
Post a Comment