JPM ahoji ubaya wake upo wapi, awakumbusha haya wafanyakazi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Tano, John Joseph Pombe Magufuli wakati akizungumza na Madiwani pamoja na Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya Chato Mkoani Geita jana amewakumbusha wafanyakazi jinsi ambavyo utawala huu unavyowalipa mishahara yao kwa wakati kulinganisha na tawala zilizopita ambapo walikuwa wakicheleweshewa mishahara yao.
”Nilipe mishahara na mishara muwe mmanapa tarehe 25 zamani mlikuwa mnafika mpaka tarehe 15 nyingine au 20 ya mwezi unaofuata mmeshasahau, Kumbe kusahau nako kwepesi wafanyakazi mmesahau mbona muda mchache tu umepita mlikuwa mnalipwa mpaka tarehe 22? ” Amehoji Rais Magufuli.
Amezungumza hayo akihoji juu ya watu wanaosema nchi inaongozwa katili na rais ni mbaya, amekumbusha baadhi ya mambo ambayo yanafanyika na mengine yamefanyika ikiwamo suala ufufuaji wa ndege za Tanzania, ujengwaji wa reli na kadhalika na kuhoji pamoja na hayo yote ubaya wake upo wapi.
”kwahiyo ndugu zangu viongozi wenzazngu najaribu kuwaeleza hili ili muelewe watakuja wengine watawaambia hii nchi katili sana huyu rais mbaya sana, ninunue meli niwe mbaya nitengeneze reli niwe mbaya, ninunue ndege ambazo mnasafiri bei imeshuka zamani kutoka dar es salaam mpaka bukoba ilikuwa mpaka milioni mbili leo mnalipa laki mbili mimi mbaya”.
Aidha Rais Magufuli kwa nafasi yake amejitahidi kwa kiasi kikubwa kushughulikia mambo ambayo yamekuwa yakipigiwa kelele na wananchi pamoja na vyama pinzani, ni wazi hawezi kufanya kila kitu au kumfurahisha kila mtu ila ukweli ni kwamba kwa ambayo ameyafanya yanaonekana na anahitaji pongezi kwa mabadiliko haya makubwa ya nchi yetu Tanzania.
Comments
Post a Comment