CCM Yawatolea Nje Wasanii Kushiriki Kwenye Shuguli za Chama Hicho
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally amesema kuwa chama hicho hakitawatumia wasanii tofauti na bendi ya TOT na Vijana katika shughuli zote za chama hicho.
Dkt. Bashiru ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha Baraza kuu la vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) jijini Dodoma ambapo amesema kuwa watafanya hivyo ili kupunguza gharama zinazokigharimu chama hicho pindi inapowalipa wasanii.

"Kuanzia sasa CCM haitatumia wasanii wa Bongo Fleva kwenye mikutano yake tutabaki na bendi yetu ya TOT. Tukienda mikoani tutawakuta wasanii wa nyimbo za asili, tunafanya hivi kupunguza gharama", amesema Dkt. Bashiru
Bendi ya TOT ilijizolea umaarufu kutokana na aliyekuwa mtunzi na muimbaji wake Kapteni John Komba ambaye kwasasa ni marehemu kuwa na mashairi yanayovutia na kuhamasisha wanachama pindi CCM inapokuwa kwenye kampeni.
Komba aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi alifariki Dunia Februari 28, 2015 katika Hosptali ya TMJ Mikocheni alikokuwa akipatiwa matibabu, hivyo kupelekea Chama hicho kutumia wasanii wa Bongo fleva na filamu katika kunogesha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Comments
Post a Comment