Waziri wa Afya Awajia Juu Wanaume "Likizo Ya Uzazi Kwa Wanaume Si Ya Kunywa Pombe’'

Waziri wa Afya: Awajia Juu Wanaume "Likizo Ya Uzazi Kwa Wanaume Si Ya Kunywa Pombe’'

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka wanaume kutoitumia likizo ya siku tano ya uzazi kwa wanaume kwenda kunywa pombe.

Aidha, amesema ataifuta likizo hiyo kwa wanaume endapo atajiridhisha haina manufaa na inatumika ndivyo sivyo.

Akizungumza kuhusu Wiki ya Unyonyeshaji itakayoanza kesho hadi Agosti 8, mwaka huu, Waziri Ummy amesema likizo hiyo ni kwa ajili ya kumsaidia mama anapokuwa amejifungua na si vinginevyo.

“Likizo ya uzazi kwa wanaume si ya kwenda kunywa pombe, lakini wapo wanaume wanachukua likizo na nyumbani hawaonekani, nitafanya utafiti kuangalia iwapo ina manufaa kama hakuna tutaifuta,” amesema.

Comments

  1. Hapana Mheshimiwa Ummy, usiifute. Ila tuwaelimishe wanaume, aslimia kubwa ni ignorant. Kwa hiyo, ina bidi tuweze darasa kwa baba mtarajiwa kuhusu hiyo likizo ina madhumuni gani na anapaswa kufanya nini katika likizo hiyo.
    Subira na Kazi yaku fundisha!
    Mchanga wangu mdogo.
    Katika kujenga Taifa letu.

    ReplyDelete
  2. Mchango wangu mdogo hapo juu. Tufanye session ya mafunzo hayo wakati mama mjamzito yuko katika mwezi wa 6. Kwasababu, just in case premature baby of 7 months is born. Kwa hiyo wafundishwe kuhusu premature babies, normal babies na mama aliye jifungua kwa upasuaji.. Nimuhim sana Ku take in consideration all circumstances.
    Ahsante.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts