Jerry Murro atwishwa migogoro ya ardhi Arumeru


Na Ferdinand Shayo, Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Meru Jerry Muro kutatua migogoro ya ardhi iliyokithiri katika wilaya hiyo na kudumu kwa miaka mirefu ikiwemo kurudisha maeneo ya serikali yaliyovamiwa na wananchi.

Akizungumza katika halfa ya kumupisha Mkuu huyo wa Wilaya ,Gambo amesema kuwa yapo maeneo ikiwemo eneo la shamba la Malula ambalo lilitengwa kwa ajili ya uwekezaji lakini wako baadhi ya wananchi wamechukua eneo hilo na kulifanya eneo la kilimo.

Gambo amemtaka kiongozi huyo kurudisha maeneo ya serikali yaliyochukuliwa kinyamela na baadhi ya watu ikiwemo kusimamia vyema maendeleo ya wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Meru Jerry Muro  amemshukuru Raisi Magufuli kwa kumteua  ili aweze kuwatumikia wananchi  na kusimamia vyema ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata maendeleo sawa sawa na dira ya Raisi.

Amewataka Wakurugenzi kusimamia vyema mapato ya serikali na kuhakikisha kuwa kila fedha ya maendeleo inatumika vizuri ili kutatua changamoto za wananchi.

Pia amewataka Wakurugenzi kuwasilisha taarifa za mapato yanmayotokana na wawekezaji wanaomiliki ardhi kubwa katika Wilaya hiyo wakiwemo wale wanaodaiwa kubadili matumizi ya ardhi.

Alisema Kuwa atasimamia vyema ilani ya chama cha mapinduzi ili wananchi waweze kupata huduma bora na stahiki


Comments

Popular Posts