Waziri Mkuu awashangaa wanaotumia mkaa wa kuni



Dar es Salaam.  Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa amesema haoni umuhimu wa wananchi kutumia mkaa wa kuni wenye gharama kubwa wakati mkaa mbadala upo kwa bei nafuu.
Majaliwa ametoa kauli  hiyo leo, Alhamisi Mei 31, 2018 wakati akizindua maadhimisho ya wiki ya mazingira katika viwanja vya Mnazi Mnazi.
Majaliwa ambaye pia ni mbunge wa Ruangwa amesema matumizi ya mkaa mbadala ni nafuu kwa maisha ya Watanzania kwani  unasaidia kuokoa ukataji wa misitu inayotumika kutengenezea mkaa wa kuni.
"Nimetembelea mabanda ya wajasiriamali wamenionyesha teknolojia ya mkaa mbadala na nimeridhika nayo. Wamenieleza mkaa huu mbadala wametengeneza kwa kutumia pumba na takataka,"amesema Majaliwa .
Majaliwa ameongeza kuwa ; "Ni vyema wakazi wa Dar es Salaam wakaja kutembelea mabanda haya na kupewa maelekezo ya namna ya kutumia mkaa huu.Huko tunakoenda mkaa wa kuni hamtauona.”
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesema hali  ya uharibifu wa mazingira  nchini bado ni mbaya na Dar es Salaam inatumia asilimia 70 ya mkaa wa kuni katika matumizi mbalimbali.

Comments

Popular Posts