VIDEO:Bunge lapitisha bajeti Wizara ya Ardhi
Dodoma. Bunge leo Jumatano Mei 30, 2018 limepitisha bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya mwaka wa fedha wa 2018/19 ya Sh73bilioni.
Bajeti hiyo imepitishwa leo katika kikao cha 40 cha Bunge la Bajeti huku mwenyekiti wa chombo hicho cha Dola, Mussa Azzan Zungu akimpongeza waziri wa wizara hiyo, William Lukuvi na naibu wake Angeline Mabula kwa utendaji wao mzuri.
Baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo ya Wizara ya Ardhii bila kupingwwa, kesho itawasilishwa bajeti ya Wizara ya Madini mwaka 2028/19, kujadiliwa kwa siku mbili.
Migogoro ya ardhi na upatikanaji wa hati za viwanja ni miongoni mwa mambo yaliyozungumzwa zaidi na wabunge katika mjadala wa bajeti hiyo.
Comments
Post a Comment