VIDEO: Rais Kenyatta, Raila wawaomba Wakenya msamaha



Dar es Salaam.Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na  kiongozi wa muungano wa Nasa, Raila Odinga leo wamewaomba msamaha wananchi kwa madhara makubwa yaliowapata kutokana na ugomvi wao wa kisiasa.
Viongozi hao waliomba msamaha leo Alhamisi, Mei 31, wakati wa hafla fupi ya 16 ya maombi ya taifa yaliofanyika jijini Nairobi.
Viongozi hao walikumbatiana na kucheka kama ishara ya kuwa wamesamehana, Rais Uhuru amesema, “Tumefanya kampeni chafu, tumedhalilishana na kuumizana, lakini leo naomba tusameheana na kuanza ukurasa mpya”
Amesema ni wakati wa kumuangukia mwenyezi Mungu na kumuomba msamaha ili kuweza kunusuru nchi yao ambayo imejikuta katika machafuko yanayopelekea vifo hasa wakati wa uchaguzi.
Amesistiza kuwa kuomba msamaha si dalili ya udhaifu bali ni dalili ya uwezo.
Amesema wamekuwa na mitizamo tofauti ya kisiasa, lakini
tofauti zao hazitaruhusiwa tena kuleta maumivu au vifo kwa wananchi.
Huku akishangiliwa na watu waliohudhuria hafla hiyo, Rais Uhuru
aliwakaribisha Makamu wa Rais, William Ruto, Odinga pamoja na mgombea mwenza wake Kalonzo Musokya kusema neno.
Kupitia fursa hiyo, Ruto naye aliwaomba wananchi wa Kenya msamaha na kuwataka kuanza safari moja yenye malengo ya amani na mshikamano.
Kwa upande wake Raila amesema, kwa niaba ya wanachama wa Nasa, anamshukuru Rais Kenyatta kwa kuweza kufikia maamuzi yenye mlengo wa kuwaunganisha na kuondoa chuki.
Amesema kitu ambacho watu hawajui, ni kuwa tangu washikane mikono, wamekuwa na mazungumzo ambayo yameangalia mambo mengi ikiwemo nini hasa kinawapelekea kugawanyika.
“Tumeamua kuungana na kufanya kazi kwa pamoja, huku tukihakikisha kuwa hakuna raia wa Kenya atakayekufa kutokana na chaguzi za kisiasa,”amesema.
Kalonzo amesistiza kuwa ni makosa wanasiasa kuchukizwa na matokeo ya uchaguzi.
“Nakiri mimi ni moja wa viongozi waliochukizwa, na matokeo hayo na matokeo yake yalikuwa hasi kwa nchi yetu,”amesema.

Comments

Popular Posts