Serikali yatakiwa kupunguza bei za viwanja Dodoma
Dodoma. Mbunge wa Mufindi Kusini (CCM) Medrad Kigola ameitaka Serikali kupunguza bei ya viwanja katika jiji la Dodoma ili kuwawezesha wananchi wengi kumiliki ardhi na kujenga nyumba za makazi.
Akizungumza katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mwaka 2018/19, Kigola amesema mita moja ya mraba inauzwa kati ya Sh 6,000 hadi Sh 12,000 jambo ambalo halimsaidii mwananchi.
“Watu wamekuja kutoka Dar es Salaam wanahangaika nyumba, nyumba hazieleweki. Kwa nini wasipunguze bei ili watu waweze kumudu maana kwa hali ilivyo mtu kupata Sh15milioni kununua kiwanja ni ngumu,” amesema.
Amesema walau Serikali ingeweka bei ya mita moja ya mraba kwa Sh3,000 na hivyo kiwanja kinaweza kuuzwa kwa Sh 2milioni.
Comments
Post a Comment