Kikwete amshukuru Kinana, amkaribisha Bashiru CCM



Dar es Salaam. Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amempongeza aliyekuwa katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa mchango wake ndani ya chama hicho tawala na kumkaribisha mrithi wake, Dk Bashiru Ally.
Kikwete ametoa pongezi hizo katika ukarasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.
Mei 29, 2018 Halmashauri Kuu, ambayo ni chombo cha pili kwa ukubwa cha CCM na ambayo ilikutana kwa siku mbili Ikulu jijini Dar es Salaam, ilimpitisha Dk Bashiru ambaye aliongoza kamati iliyohakiki mali za chama hicho kwa miezi mitano kuwa katibu mkuu mpya wa chama hicho.
Mhadhiri huyo wa Sayansi ya Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) amechukua nafasi ya Kinana aliyejiuzulu baada ya kuwasilisha maombi kwa mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli.
Katika ukurasa wake huo Kikwete amesema, “kwa heri Kinana hongera kwa kazi nzuri daima tutakukumbuka. Hongera Bashiru nakutakia kila la heri.  Hongera CCM, hongera mwenyekiti Magufuli, umoja ni ushindi. Kidumu chama cha mapinduzi.”

Comments

Popular Posts