Ahadi kwa wananchi zamtesa Mtulia, ambana Lukuvi bungeni

Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia akizungumza

Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia akizungumza bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka wa fedha 2018/2019, jijini Dodoma leo.

Dodoma.  Mbunge wa Kinondoni (CCM), Maulid Mtulia amemtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvu kueleza mkakati upi aliondaa wa kulifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa jiji jipya.
Akizungumza leo Mei 30, 2018 bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mwaka 2018/19, Mtulia amesema wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, Februari 2018 aliahidi Dar es Salaam mpya kwa wananchi, hasa Mto Msimbazi unaogeuka kero kwa wananchi zinaponyesha mvua kubwa.
“Tulipoikuwa katika kampeni tulizungumzia Dar es Salaam mpya, waziri (Lukuvi) uje na mkakati wa kulifanya jiji la Dar es Salaam kuwa Dar es Salaam mpya tukisema wanaoishi mabondeni wavunjiwe kwa hiyo zaidi ya asilimia 60 ya nyumba tutazivunja,” amesema Mtulia.
Amesema kwa sasa Dar es Salaam ina wakazi zaidi ya milioni sita na ikitokea wananchi wa mabondeni wakavunjiwa nyumba zao maana yake asilimia 60 ya nyumba zitabomolewa.
Amebainisha kuw ahaiwezekani kwa jiji hilo shughuli kusimama kila mvua kubwa inaponyesha huku Mto Msimbazi ukiwa chanzo na kubainisha kuwa kama watatokea wawekezaji na kutaka kuwekeza katika mto huo waruhusiwe.

Comments

Popular Posts