JPM amteua Dk Mafumiko kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali
Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Dk Fidelice Mafumiko kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali.
Uteuzi huo wa Dk Mafumiko umeanza leo Jumanne Aprili 3, 2018.
Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa kabla ya uteuzi huo, Dk Mafumiko alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW).
Dk Mafumiko anachukua nafasi ya Profesa Samuel Manyele ambaye amemaliza muda wake.
Comments
Post a Comment