Majaliwa awataka wakandarasi kununua mabomba nje ya nchi
Mwanza. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hakuna sababu ya wakandarasi wa miradi ya maji kuagiza mabomba nje ya nchi wakati kuna mabomba yanayozalishwa hapa nchi tena kwa ubora hivyo kuwataka watumie ya ndani .
Ameyasema hayo Februari 20 wakati akiweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kuzalisha mabomba cha Mwanza Plstics eneo la Nyamhongolo wilayn Ilemela Mwanza.
"Niwatake wakandarasi tuendelee kutumia mabomba ya ndani ili kuendelea kutoa sapoti kwa wawekezaji hawa,"amesema
Kwa kusimamia hilo ameagiza miradi yote ya maji inayotekelezwa katika halamshauri za mkoa huo kuhakikisha mabomba ya maji yananunuliwa katika kiwanda hicho cha mzawa ilmradi kiwango cha mabomba hayo yawe yanapatikana hapo.
"Kuna mradi wa kusambaza maji katikati ya mji wa Sh14 bilion ambao upo hatua za manunuzi, mkurugenzi wa Mwauwasa simamia hilo wakandarasi wanunue mabomba kiwanda hiki," amesema Waziri
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho John Charles alisema kiwanda hicho chenye wafanyakazi 15 wazawa wenye ajira za kudumu na watatu kutoka nje ya nchi, kilianza mwaka 2008 kwa kutengeneza plastiki na vikombe.
Amesema wanakabiliwa na uhaba wa umeme wa kutosha kwani unakuwa wakati mwingine unakosa nguvu na miundombinu ya barabara hivyo kuonheza gharama za uzalishaji.
Kutokana na hayo waziri alimwagiza mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela John Wanga kuhakikisha maeneo yote ya uwekezaji kuhakikisha miundiombinu yote muhimmu inafika.
Comments
Post a Comment