Je Korea Kaskazini na Korea Kusini wamekua marafiki tena?

Timu ya Korea ikijiandaa kukabilia na timu ya Sweden katika awamu ya kwanza ya mpira wa magongo wa barafuni katika siku ya tatu ya michezo ya Olyimpiki ya majira ya baridi mjini PyeongChang 2018Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTimu ya mpira wa magongo ya wanawake ya Korea ilijumuisha wachezaji kutoka Korea Kusini na Kaskazini
Taarifa kubwa ya Olimpiki ya majira ya baridi mwaka 2018 nchini Korea Kusini imekuwa ni maneno ya urafiki baina ya mataifa hayo mawili. Imewafanya wengi wajiulize je, Olimpiki itaboresha daima uhusiano baina ya nchi hizo mbili?
Wakati michezo hiyo ilipoanza mjini Pyeongchang wanariadha wa Korea Kaskazini na Korea Kusini, walitembea kwenye sherehe za ufunguzi kwenye kikundi kimoja kama timu moja.
Ulikuwa ni wakati wa kuonyesha ishara yao ya umoja, huku wakibeba kwa pamoja bendera yenye rangi moja ishara ya "inayounganisha rasi ya Korea''.
Halafu, Kim Yo-jong - dada yake Kim Jong-un - akaenda katika kile kinachoitwa Olimpiki charm Offensive, ambapo timu ya pamoja ya Korea Kaskazini na Kusini ya mpira wa magongo wa kwenye barafu ilikua ikicheza na kikosi cha mashabiki wa Korea Kaskazini kutoka maeneo mbali mbali ya dunia kikashangilia.
Lakini je hali iliyojitokeza wakati wa Olimpiki itadumu?
Matarajio ya kuendelea kwa hali hii kutokana na maneno ya kirafiki yaliyokuwa yakitolewa na pande mbili yamepewa uzito.
Kutangazwa kwa habari hizi kwa mapana zaidi katika vyombo vya habari vya Korea hizo mbili na kwingineko duniani kumeonekana kama mafanikio makubwa ya uhusiano baina ya pande mbili vyombo huru vya habari vya Korea Kusini vimesema kuwa ''Moyo wa Olimpiki'' umelainisha mazungumzo na Korea Kaskazini na utawala huria wa rais Moon Jae-in.

Lakini si kila mmoja anafurahia.

Mahafidhina wamekasirika sana, kwamba uhariri katika vyombo vya habari vya mrengo wa kulia na kushoto mara kwa mara umekua ukitoa madai dhidi ya kukubaliana kila kitu cha Pyongyang katika mazungumzo yoyote.
Hofu moja ni kwamba Korea Kaskazini inaweza kuomba iachane na mafunzo ya pamoja ya kijeshi ya Korea Kusini na Marekani kutokana na ahadi za kuangamiza mipango yake ya makombora ya masafa marefu pamoja na nuklia jambo ambalo inajua kwamba italikiuka.
Ukweli ni kwamba matarajio yanaweza kukiukwa kwa pande zote mbili kwa nchi hizi kuendelea na mambo kama yalivyo sasa na hilo ndilo linalotarajiwa zaidi.
Tukio hili la michezo huenda lisihimili vishindo vya uhasama mkubwa uliopo baina ya Korea hizi mbili..
Mazungumzo ya miongo kadhaa bado hayajaleta maridhiano, na linalotia shaka zaidi ni kusikia maneno matamu kupita kiasi kutoka pande mbili, hali inayoashiria kwamba uhusiano utarejea katika hali ya kawaida.
Hali ya mahusiano imekua si ya kubadilika kwa Korea Kaskazini tangu mwishoni mwa vita vya Korea miaka 65 iliyopita.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in (katikati) akitazama mchezo wa Olyimpiki na dada yake kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-in , Bi Kim Yo-jong (Kushoto) tarehe 11 Februari, mjini Seoul, Korea Kusini.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKim Yo-jong, dada yake kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, akitazama mchezo na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in
Korea Kaskazini bado inadaiwa kuwa ndio taifa hatari zaidi duniani, mpango wake wa silaha za nuklia ukizidisha vitisho .
Uwezekano wa mazungumzo inapoonyesha utashi kama ilivyofanya ghafla mwezi Januari -kila mara huongeza matumaini kwa dunia ambayo haijui ifanye nini kuhusu kumaliza tatizo hilo bila kutokea machafuko.
Inapokuja katika mazungumzo wakorea wa Kaskazini ni wagumu sana.
Hupigania kila pendekezo lao na kuhakikisha wamelidondoa na kulielezea kwa mapana na marefu.
Na kila maafikiano wanayofanya na Marekani na Korea Kusini huhakikisha yamefafanuliwa kwa mapana iwezekanavyo , huku jambo lolote linaweza kutarajiwa kwao kuwa dogo sana.
Utekelezaji wa mikataba na Korea Kaskazini umekuwa ni wa kudorora kutokana na masuala madogo kama vile ya ufafanuzi na muda.
Uwezekano wa kwamba michezo ya Olimpiki italeta mwamko wa maafikiano ama ushirikiano na Pyongyang ni wa kiwango cha sifuri.
Ikiwa hilo litawezekana basi itakuwa ni miujiza kwani itakuwa ni kinyume kabisa na tabia ya mazungumzo ya nyuma ya utawala.
mara kwa mara Korea Kusini huingalia Kaskazini kama jamii ya ndugu zao ambao walitengwa nao kwa njia isiyo ya haki kupitia Vita Baridi.
Marekani pia haitafurahia iwapo nchi hizi zitakuwa na mahusiano mema, hasa kutokana na uhasama uliopo baina ya utawala wa rais Trump na Korea Kaskazini
Rais wa Korea Ksuini Kim Dae-jung, kushoto, na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong- wakishiriki kinywaji nchini Korea Kaskazini mwaka 2000Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais wa Korea Kusini Kim Dae-jung, kushoto, na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong- wakishiriki kinywaji nchini Korea Kaskazini mwaka 2000
Rais Moon anaweza kwenda Pyongyang katika miezi ijayo, kutokana na mwaliko alioupokea kwa mikono kutoka kwa Kim Yo-jong wakati wa michezo ya Olimpiki mjini Seoul.
Ingawa bado hapajawa na makubaliano rasmi, Bwana Moon alisema wakorea wanapaswa "kuhakikisha hilo linafanyika" na kuwatolea wito Korea Kaskazini kurejea kwenye meza ya mazungumzo na Marekani.
Hata hivyo mazungumzo si suluhu ya uhasama baina ya nchi hizi mbili.
Mazungumzo ya awali yalivunjika kutokana na uhasama huo.
Timu ya Korea ikijiandaa kukabilia na timu ya Sweden katika awamu ya kwanza ya mpira wa magongo wa barafuni katika siku ya tatu ya michezo ya Olyimpiki ya majira ya baridi mjini PyeongChang 2018Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTimu ya mpira wa magongo ya wanawake ya Korea ilijumuisha wachezaji kutoka Korea Kusini na Kaskazini
Jambo tofauti wakati huu ni kwamba Korea Kaskazini itafikia makubaliano katika moyo wa Olimpiki ili kuanzisha mazungumzo na kuepuka mtazamo wa dunia wa kutokua na nia ya kumaliza uhasama na Korea Kusini
Lakini kuna uwezekano mkubwa kwamba itajaribu kadiri iwezavyo kuitenganisha Korea Kusini na Marekani, ikiichezea shere Korea Kusini kutokana na chuki yake kwa Donald Trump
Kuna uwezekano pia kwamba itatoa madai ambayo inafahamu fika kwamba Korea Kusini haitayatimiza, kama vile ombi lake la hivi karibuni la kuwarejesha watoro.
Huku matumaini yamesalia kwamba mambo yatakuwa tofauti baada ya Olimpiki.Ukweli ni kwamba ni bora watu wasiwe na matumaini makubwa.

Comments

Popular Posts