RC Makonda Awatangazia Kiama Wafanyabiashara


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuanzia Jumatatu ya June 03 mwaka huu ni marufuku kwa Wafanyabiashara wadogo (Machinga) ndani ya mkoa huo kufanya biashara bila vitambulisho maalumu vya utambuzi vilivyotolewa na Rais Dkt. John Magufuli.

Amesema kuwa kuanzia Jumatatu ataanza msako wa kuwakamata wafanyabiashara wasiokuwa na vitambulisho ndani ya jiji la Dar es salaam kwakuwa walipatiwa muda wa kutosha wa kujisajili na kupatiwa vitambulisho hivyo vya Ujasiriamali.

Aidha, hatua hiyo imekuja mara baada ya Makonda kubaini uwepo wa wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao bila kuwa na vitambulisho na hiyo ni baada ya kufanya ziara katika mitaa 9 na kubaini kuwepo kwa wafanyabiashara wengi wanaofanya shughuli zao bila vitambulisho vya ujasiriamali jambo ambalo sio matarajio ya serikali.

Hata hivyo, kutokana na hilo amewataka wafanyabiashara wasiokuwa na vitambulisho kufika ofisi za wakuu wa wilaya ili waweze kusajiliwa na kupatiwa vitambulisho.

Comments

Popular Posts