Dhana potofu kuhusu dengue
Aprili mwaka huu, Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ilitangaza rasmi uwapo wa mlipuko wa ugonjwa dengue nchini hasa Mkoa wa Dar es Salaam, huku idadi ndogo ikiwa Tanga na Singida.
Hadi sasa vifo vichache vilivyotokana na ugonjwa huo vimeripotiwa, lakini tumeshuhudia baadhi ya ndugu na marafiki zetu wakiugua dengue.
Kwanza kabisa nianze na kuishukuru Serikali kupitia wizara husika, madaktari na wataalamu wengine wa afya ambao kwa wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kutoa elimu kadri iwezekanavyo ili kuhakikisha kila mwananchi anapata uelewa kuhusiana na ugonjwa huu na afahamu namna ya kujikinga.
Hii imesaidia kuwafanya watu wapate angalau wapate uelewa kuhusu dengue.
Siku hizi neno dengue siyo geni kwa mtu yeyote; hii inaonyesha ni kwa namna gani wananchi wameelewa kuhusiana na tatizo hili.
Pia, kama ilivyo kawaida linapoz uka jambo na elimu kutolewa, kila mmoja ataelewa kwa namna tofauti na kutafsiri anavyojua.
Nimekuwa nikiwahudumia wagonjwa wengi wa dengue katika hospitali ninayoifanyia kazi, lakini kila mgonjwa ninayemuhudumia, amekuwa na uelewa na dhana tofauti ninapokuwa nazungumza naye kuhusiana na ugonjwa huu.
Hivyo basi, tukiwa bado tunaendelea kupambana na ugonjwa huu ambao bado umekuwa ukiwapata watu, nimeona ni bora leo nikakukumbusha baadhi ya dhana potofu ambazo wengi wanazo kuhusu dengue.
Baadhi ya watu hudhani ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mwingine, hii ni moja ya dhana ambayo inapaswa kupuuzwa.
Nimeshuhudia zaidi ya mara moja, wagonjwa wangu wanaogopa kurudi nyumbani kwa madai kuwa wanaweza kuwaambukiza watu wao wa karibu kwa njia ya hewa au kwa kushirikiana kwa namna yoyote ile.
Comments
Post a Comment