Rapper Nipsey Hussle amepigwa risasi na kufariki asubuhi ya kuamkia leo, jijini Los Angeles nchini Marekani, wakati akitoka dukani kwake

Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali na vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti juu ya kifo cha rapa Nipsey Hussle aliyepigwa Risasi mbele ya duka lake la Mavazi Marathon Clothing. 

Ripoti ya Polisi inasema Nipsey alishambuliwa na Risasi kadhaa mwilini mwake na Alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa Hospital. 
Jina kamili la Nipsey ni Ermias Davidson Asghedom alikulia Los Angels na miaka ya 90 Alijihusisha na makundi kadhaa ya Uhalifu. 
Mapema siku ya Jana kupitia mtandao wake wa Twitter alitwit hivi “Having Strong Enemies is a blessing.” Yaani Kuwa na Maudui wenye ngungi ni baraka. 
Polisi nchini Marekani bado haijatoa ripoti kamili juu ya mauaji hayo. 

Comments