Chunya imebadilika kiuchumi– Magufuli

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amesema Chunya ya mwaka 2015 siyo ya sasa kutokana na kuwepo kwa mabadiliko ya kiuchumi na kuongezeka kwa makazi bora.
Ameyasema hayo leo Aprili 27 katika mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Sabasaba wilaya ya Chunya mkoani Mbeya ikiwa ni muendelezo wa ziara yake mkoani humo.
“Vile vijiji ambavyo zamani havikuwepo sehemu ilikuwa inaonekana ni maporini au nyumba ziko mbalimbali leo vimekuwa vijiji vikubwa hongereni sana.”
“Nakumbuka nikiwa Waziri wa miundombinu nilipokuwa nikitoka Mbeya kuja huku ukikutana na wananchi barabarani wakikuangalia wanaonyesha kabisa jinsi gani wamechoka na wanakuonyesha chini barabara kuwa wanahitaji kujengewa barabara.”
“Na mmesikia kuwa ujenzi wa barabara hii kutoka Mbeya hadi Chunya umegharimu Sh139.99 bilioni huku ujenzi wa barabara ya Chunya Makongolosi ukigharimu Sh62.67 bilioni hizi ndiyo ahadi nilizowapa, nazitekeleza,” amesema Magufuli.

Comments
Post a Comment