Rayvanny awachezeha wimbo wa Tetema, Waziri Kigwangala na Manara, achemka kwa RC Makonda (+ Video)
Katika kampeni ya Tokomeza Zero iliyoandaliwa na DC wa Kisarawe Mh. Joketi Mwegelo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Mlimani City walihudhuria viongozi mbalimbali wa Serikali lakini pia pamoja na wadau mbalimbali wa Sanaa ikiwemo wasanii na hata watu ambao sio wasanii ila wana umaarufu.
Katika hafla hiyo walifanikiwa kuongea viongozi mbalimbali na wadau mbalimbali katika kutoa ahadi ya kuchangia angalau chochote walichojaliwa nacho kwa ajili ya kupata pesa zitakazo saidia kujenga shule ya kwanza ya bweni ya wasichana katika wilaya hiyo ya kisarawe na kuna baadhi ya wasanii walipata nafasi ya kupafomu mmoja wao akiwa Rayvanny na OmmyDimpoz lakini Rayvanny alifanikiwa kufanya zoezi la kuwachezesha wimbo wa Tetema watu mbalimbali na kwa Waziri Kigwangala na Haji Manara alifanikiwa ila alipofika kwa RC Makonda aligonga mwamba.

Comments
Post a Comment