Mkuu wa Wilaya ya Newala Apata Ajali Mbaya ya Fari



Mkuu wa Wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo na watu wengine watatu wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa wamepanda kupata ajali na kupinduka.

Tukio limetokea eneo la Mandawa juzi saa mbili usiku wilayani  Kilwa Mkoa wa Lindi  wakati mkuu huyo akiwa safarini kwenda Dar es Salaam.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine, Muhaji Mohamedi  amesema amepokea majeruhi wanne  ambao ni Aziza Mangosongo, Mwanahamisi  Naenda, mkazi wa Kitangali, Zaituni Lipau  na Jasiri Nguru.

Amesema wanatarajia kuwapa rufaa majeruhi kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  kwa matibabu  zaidi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatus Chalya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema dereva Daudi  Kakulilo wa gari hilo la Serikali anashikiriwa  na polisi kwa mahojiano.



                     KWA HABARI ZA MICHEZO PAKUA APP YETU YA MICHEZO SASA


Comments