Swali la adhabu ya viboko kwa wanafunzi 'lawasha moto' Bungeni .....Spika Ndugai Asema Hata Yeye Amewahi Mtandika Mtu Viboko
Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema bila viboko shuleni mambo hayaendi vizuri. Amesema hata yeye amewahi mtandika mtu viboko.
Spika amesema hayo Jana Alhamisi Januari 31, bungeni jijini Dodoma baada ya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, kusema viboko vitaendelea kutumia shuleni.
Ole Nasha alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Zainab Katimba.
Katika swali lake Katimba alitaka kujua kama adhabu ya viboko inaongeza kiwango cha ufaulu.
Akijibu swali hilo, Ole Nasha amesema Serikali itaendelea kusisitiza matumizi sahihi ya adhabu kwa wanafunzi ili kuleta tija katika ufundishaji na ujifunzaji.\
==>>Tazama hapo chini
Comments
Post a Comment