Ripoti ya Mo Ibrahim yaipa hadhi Tanzania katika utawala bora.



TANZANIA imeshika nafasi ya 14 kati ya nchi 54 za kiafrika katika ripoti ya mwaka huu, iliyotolewa na taasisi ya ‘Mo Ibrahim Foundation’ kuhusiana na masuala mbalimbali ya kiutawala na kijamii.
Masuala yalioangaziwa katika ripoti hiyo iliyojumuisha nchi zote barani Afrika, ni pamoja na usalama wa raia na utawala wa sheria, ushiriki katika haki za binadamu, uchumi imara, fursa pamoja na maendeleo ya binadamu.
Katika maelezo ya awali kwenye ripoti hiyo iliyofanyiwa utafiti mwaka jana 2017, Ibrahim alisema nchi nyingi za kiafrika kwa sasa zinapiga hatua katika maendeleo ingawa zipo ambazo zimesimama palepale kutokana na aina ya uongozi walionao.
“Utawala wa sheria na haki za binadamu ndiyo kitu cha msingi katika kuleta mabadiliko kwenye serikali za kiafrika, bado kuna baadhi ya mataifa yapo nyuma katika sekta hii lakini kuna maeneo wameendelea,” alisema Ibrahim katika utangulizi wa ripoti hiyo.
Alibainisha, yapo mataifa yamefanya mabadiliko ya haraka katika utawala ingawa kuna upinzani mkubwa umetolewa kutoka katika baadhi ya taasisi za ndani na nje ya Afrika.
“Mabadiliko chanya makubwa yametokea katika ripoti ya mwaka huu, mataifa 15 kati ya 34 yameonyesha maendeleo makubwa ya kiutawala ndani ya muongo mmoja, wengine ndani ya miaka mitano wamefanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi.
“Miongoni mwa hizo ni Ivory Coast, Morocco na Kenya ambazo zimeonyesha maendeleo ya kuvutia, zimehama kutoka nafasi za 41, 25 na 19 hadi nafasi ya 22, 15 na 11 ndani ya muongo mmoja,” alisema Ibrahim na kuongeza:
“Kwa ujumla kwenye bara zima, viashiria vya mabadiliko vinaonekana kwenye sekta muhimu ikiwemo afya na miundombinu. Vilevile kuna mabadiliko makubwa ya hivi karibuni kwenye utawala wa sheria, uwazi na uwajibikaji katika kazi.”
Nchi zilizoongoza ni Mauritius ambayo imeshika namba moja ikifuatiwa na Shelisheli, Cabo Verde (3), Namibia (4), Botswana (5), Ghana (6), Afrika Kusini (7), Rwanda (8), Tunisia (9), Senegali (10), Kenya (11), Sao Tome & Principe (12), Benin (13) na Tanzani nafas ya 14.
Aidha, ripoti hiyo imeiweka Tanzania katika nafasi ya 10 kati ya nchi zenye ukuaji mkubwa wa pato la taifa (GDP) barani Afrika, ambapo kwa mwaka jana ilionyesha ina GDP ya Dola za Marekani 52,090 ikiwa inaongozwa na Nigeria yenye Dola 375,771, afrika Kusini (Dola 349,419), Misri (Dola 235,369), Algeria (Dola 170, 371), Angola (Dola 124,209), Sudan (Dola 117,488), Morroco (Dola 109, 139), Ethiopi (Dola 80,561) Kenya (Dola 74,938) na mwisho ni Tanzania.
Matokeo haya ni ya 12 tangu utaratibu huu uanzishwe mwaka 2007, ambapo ripoti ya mwaka huu imeonyesha mabadiliko makubwa katika bara la Afrika hasa katika upande wa utawala bora ambao ukuajiw ake unaridhisha. Ambapo watu watatu kati ya wanne wanaishi kati mataifa ambayo utawala bora umeimarika ndani ya muongo mmoja.
             Application ya CCM NEWS Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi   
 

Comments