Ndugu Wabaini Ndugu yao Yupo Hai Baada Kukabidhiwa na Hospitali Akidaiwa Amekufa
KIGOMA: Ndugu wabaini binti yao yupo hai muda mfupi baada ya kukabidhiwa mwili wa binti huyo kwa hatua za mazishi ikiwa ni baada ya daktari kuthibitisha kifo chake
Binti huyo, Selina Michael(17) mkazi wa mtaa wa Butunga alipelekwa katika hospitali ya Baptist kupata matibabu na baadae familia kuarifiwa na Mganga wa zamu kuwa binti huyo amefariki
Wazazi wa binti huyo wameeleza kuwa chanzo cha binti huyo kupelekwa hospitali ni baada ya kuanguka ghafla alipokuwa akishuhudia vurugu zilizokuwa zikiendelea nyumba ya jirani
Aidha, Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali hiyo, James Chausa amekiri kumpokea binti huyo na kwamba Mganga wa zamu wa siku hiyo Cassian Ndilaliha alimpima na kubaini kuwa tayari amekwishapoteza maisha
Inadaiwa kuwa binti huyo alipoteza maisha kwa nguvu za giza na wakati daktari anampima hakuwa na mapigo ya moyo

Comments
Post a Comment