Mazungumzo ya Lugola, Lugumi yaanza
Mmiliki wa kampuni ya Lugumi, Said Lugumi (kulia) akiwa na mwanasheria wake, Onesmo Mpinzile wakitoka katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam leo baada ya kufanya mazungumzo na waziri wa wizara hiyo, Kangi Lugola.
Dar es Salaam. Mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola na mmiliki wa kampuni ya Lugumi, Said Lugumi yameanza muda huu katika ofisi za wizara hiyo jijini hapa.
Leo asubuhi Julai 31, 2018 Lugumi alifika katika ofisi hizo kuitikia wito wa Lugola ambaye Julai 21, 2018 alimpa siku 10 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro kumfikisha ofisini kwake mmiliki huyo wa kampuni ya Lugumi.
Mazungumzo hayo pia yamehudhuriwa na katibu mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu; naibu katibu mkuu, Ramadhan Kailima na baadhi ya maofisa wa polisi.

Comments
Post a Comment