Watanzania watakiwa kubadilika matumizi ya bidhaa

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Mpoki


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya 
Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya amewataka wananchi kusoma maelezo yaliyoandikwa kwenye bidhaa wanazotumia ili kuepuka matumizi ya kemikali hatarishi.
Dk Ulisubisya amesema hayo Juni 28, 2018 kwenye mjadala wa Jukwaa la Fikra kuhusu maradhi  yasiyoambukiza.
Amesema hayo akizungumzia ushauri uliotolewa na mmoja wa wachangiaji wa mjadala huo aliyependekeza yawekwe maelekezo ya kiwango cha sukari kilichopo katika bidhaa.
Katibu mkuu amesema ni vizuri wananchi wakawa makini kusoma kile kilichoandikwa kwenye bidhaa wanazotumia.
“Changamoto ni kuwa wengi hawapendi kusoma,” amesema.
Dk Ulisubisya amesema, "Madhara ya sigara yameandikwa tena kwa herufi kubwa lakini mtu ananunua na anavuta tu. Na wengi wetu hatusomi hata maelezo yaliyopo kwenye juisi tunazokunywa.”
Amesema wazo la kutoa tahadhari ni zuri na hasa kwa bidhaa za sukari, sigara na mafuta.


Comments

Popular Posts