Sababu Rais wa Zimbabwe kuzuru Bagamoyo




Dar es Salaam. Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa leo Juni 29, 2018 ametembelea Chuo cha Sanaa cha Wazazi Kaole Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Majengo ya chuo hicho yalitumika katika mafunzo ya kijeshi ya wapigania uhuru wa nchi za kusini mwa Afrika, rais huyo alikuwa mmoja wa walioshiriki mafunzo hayo.
Katika ziara hiyo, Mnangagwa ameongozana na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi.
Rais huyo wa Zimbabwe aliwasili nchini jana Juni 28 kwa ziara ya siku mbili na kufanya mazungumzi na mwenyeji wake Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Leo mchana anatarajiwa kurejea Zimbabwe.
Katika mazungumzo yao, wawili halo wamekubaliana kuboresha ushirikiano katika uwekezaji, biashara na utalii.
Ziara ya Mnangagwa ni ya kwanza tangu alipochaguliwa kuwa rais za Zimbabwe baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe kujiuzulu.
Leo mchana rais huyo ameondoka kurejea Zimbabwe.


Comments

Popular Posts