Mbunge ataka wanaume ‘wazee’ wakopeshwe

Mbunge wa Kavuu, Pudensiana Kikwembe akiuliza

Mbunge wa Kavuu, Pudensiana Kikwembe akiuliza swali katika kikao cha 43 cha mkutano wa Bunge la Bajeti, jijini Dodoma leo. 
 Mbunge wa Kavuu (CCM), Dk Pudensiana Kikwembe ameitaka Serikali kulegeza masharti katika ukopeshaji ili iweze kuwakopesha wazee na wanaume ambao hawaangukii katika kundi la akinamama na vijana
Dk Kikwembe ameyasema hayo leo Jumatatu Juni 4, 2018, bungeni na kuomba Serikali kutoa maelezo kwa kuwa hakuna sheria maalumu inayowabagua, lakini cha kushangaza halmashauri zinabagua makundi hayo
Katika swali la msingi mbunge huyo amehoji kuwa Serikali haioni kuwa sharti la kujiunga kwenye vikundi ili wananchi waweze kukopeshwa linawanyima fursa baadhi ya wananchi ambao pengine wanahitaji huduma.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Antony Mavunde amesema utoaji wa mikopo kwa kutumia vikundi ni mfumo ambao hutoa mikopo midogomidogo kwa ajili ya shughuli za uzalishaji mali.
“Mfumo huu hutumika kutoa mikopo kwa watu ambao uchumi wao ni mdogo hasa kwa wakopaji ambao hawana dhamana. Pia husaidia kuweka dhamana mbadala ya usalama wa mikopo inayotolewa kwa kuwafanya wana kikundi kuwa na uwajibikaji wa pamoja juu ya mkopo huo,” amesema Mavunde.

Comments