MBOWE ATAJA VIPAUMBELE BAJETI YA UPINZANI

Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, Halima Mdee


Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, Halima Mdee akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, jijini Dodoma leo. 
Dodoma. Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, Halima Mdee amesema kwa mara ya kwanza watasoma bajeti ya upinzani bungeni Jumatatu Juni 18, 2018.
Aprili, 2018 kambi ya upinzani iliazimia kutowasilisha hotuba za bajeti na nyingine za upinzani hadi watumishi wa sekretarieti yao ambao mikataba yao hutolewa na Bunge watakaporejeshwa kazini.
Akizungumza na waandishi wa habari, leo Juni 16, 2018 jijini Dodoma, Mdee amesema watasoma bajeti yao ili kuwaonyesha Watanzania bajeti mbadala ya upinzani.
“Kama mnavyojua, tumekuwa hatusomi bajeti zetu, lakini kwa mara ya kwanza tutasoma bajeti ya upinzani bungeni Jumatatu,” amesema Mdee.
Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe (Chadema), amesema bajeti hiyo itabainisha masuala mbalimbali ambayo Serikali imeshindwa kuyapa kipaumbele.

Comments