Marufuku Mtumishi Kulala na Gari ya Serikali Nyumbani kwake- Waziri Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wanaoishi nje ya eneo lao la kazi wawe wamehamia ifikapo July 30, mwaka huu.
“Tunataka watumishi wa umma wawajibike na waishi katika vituo vyao vya kazi. Nawataka watumishi wote wa wilaya hii wanaoishi Dodoma wawe wamehamia hapa ifikapo July 30 mwaka huu na wasiohamia nipewe majina yao,” amesisitiza Majaliwa
Pia ameagiza magari yote ya Serikali baada ya kuisha muda ya kazi yawe yameegeshwa kwenye ofisi za halmashauri na ni marufuku kwa magari hayo kulala nyumbani kwa mtu.

Comments
Post a Comment