Rais Magufuli akutana na Shein, Mangula Ikulu



Dar es Salaam. Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Ali Mohamed Shein.
Shein ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alikutana na Rais Magufuli jana katika kikao ambacho, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Philip Mangula alihudhuria pia.
Taarifa iliyoletwa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu leo Mei 26, imesema mazungumzo ya viongozi hao yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
“Viongozi hao wamezungumzia masuala mbalimbali yahusuyo chama na Serikali.” Imesema taarifa hiyo

Comments